RAZUKU YA THRIVE
Ruzuku ya Thrive , hufadhili mipango kazi inayounda mfumo wa haki kwa wanyama na ya chakula inayotegemea mimea, kwa kupunguza ulaji/matumizi ya vyakula vitokanavyo na wanyama na kupunguza ufugaji wa wanyama wengi kwenye eneo dogo au uwakili wa ulaji vyakula vitokavyo na mime.
Tunaomba maombi yote yatumwe kwa lugha ya kiingereza.
Kuhusu Ruzuku ya Thrive
(Asante kwa mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji ya Thrive Africa, Dk. Nathan Leonard, kwa tafsiri.)
Ruzuku ya Thrive huwa kati ya $10,000 hadi $50,000 dola za Marekani, Ruzuku ya Thrive imeelekezwa kwa taasisi zenye uwezo wa kati au mkubwa zenye historia nzuri ya mafanikio. Tafadhari tazama ruzuku nyinginezo hapa. www.thrivephilanthropy.org/grants
Tarehe za mwisho kuomba ruzuku kila muhula ni saa 5:59 usiku (GMT) mwezi
Machi 1
Juni 1
Septemba 1
Disemba 1
Baada ya kutuma maombi ya ruzuku, huchukua muda wa hadi wiki 8 ili kujibiwa, ingawa lengo letu ni kutoa ruzuku kwa waombaji wengi kadri inavyowezekana, upatikanaji wa ruzuku bado ni mdogo, hivyo kwa bahati mbaya sio waombaji wote huweza kupatiwa ruzuku.
Tafadhali telezesha chini ili kusoma vigezo stahiki vya kuomba ruzuku.
Kwa wakati huu taasisi zilizopo Marekani au taasisi za kimataifa kutoka nchini Marekani hazistahiki ruzuki hizi. Mapendekezo ya miradi yanakaribishwa kupitia fomu ya mtandaoni. Kwa bahati mbaya hatupokei maombi ya ruzuku kwa njia ya barua pepe. Kimsingi taasisi moja inaweza pokea ruzuku moja tu kwa mwaka.
Usawa ni nguzo yetu katika utoaji wa ruzuku ,Miradi inayoongozwa na wanawake, watu wa rangi, watu waliotengwa au wenye ushawishi mdogo kwenye jamii wanasisitwa kuomba ufadhili wa ruzuku.
Je una swali? tuandikie kupitia info@thrivephilanthropy.org
Tunaomba maombi yote yatumwe kwa lugha ya kiingereza
Angalizo maalum kwa taasisi zinazoomba ruzuku kutokea Afrika:
Ikiwa taasisi yako iko Afrika, na unawiwa kuomba ufadhili, na hujawahi kupokea ufadhili wa ruzuku kutoka Thrive hapo kabla, tunakukaribisha kujiunga na programu ya jenga uwezo ya Thrive HAPA. Ndani ya programu ya jenga uwezo utakutana na wadau wenye nia moja kama wewe, ambao ni mawakili kutoka afrika. Lakini pia kujiunga pamoja kutasaidia Thrive kukufahamu wewe pamoja na kazi zako, kisha Thrive itakualika kuomba ufadhili wa ruzuku ya mbegu. Kisha ikiwa utapokea ruzuku ya mbegu, utakuwa umejitengenezea kigezo cha kustahiki ruzuku ya Thrive hapo baadae.
Kwa sababu ya kiasi kikubwa cha maombi ya ufadhili wa ruzuku kutoka Afrika, maombi haya ya ruzuku kutoka Afrika huweza kukubaliwa kutoka kwa washiriki wa programu ya jenga uwezo ya Thrive Afrika, wapokeaji wa ruzuku waliopita, na kwa wale waliotumiwa mrejesho wa kuomba ufadhili. Tunashukuru kwa kuelewa.
Vigezo Stahiki
Maombi ya ruzuku yanayolenga mfumo wa haki kwa wanyama, mfumo wa vyakula vitokananyo na mimea kwa kupunguza ulaji wa wanyama ulimwenguni, kupunguza mfumo wa ufugaji wa wanyama wengi kwenye eneo dogo, au uwakili wa ulaji vyakula vitokanavyo na wanyama.
Kuendana na sera ya nafasi salama ya Thrive Philanthropy
Taasisi iwe nje ya nchi ya Marekani au/isiwe sehemu/tawi la taasisi ya kimataifa iliyoko nchini Marekani
Waombaji wote inawapasa kuonesha kuwa wakati wote wako katika mahusiano chanya na wadau pamoja na jamii inayowazunguka, na wanaweza kuchangia ukuaji chanya wa Thrive Philantthropy
Iwe taasisi isiyotengeneza faida
Kwa sasa tunatoa kipaumbele kwa taasisi zenye bajeti chini ya $ 500,000 dola za Marekani
Miradi isiyostahiki
Uzalishaji wa nyama utokanao na seli za wanyama
Miradi au taasisi zinazonufaika , kusaidia au kijihusisha na unyonyaji kwa wanyama au binadamu
Taasisi au miradi inayotoa vitendea kazi ,misaada au misaada ya vyakula vitokanavyo na mimea kwa polisi au jeshi
Taasisi zinazotengeneza faida ikiwemo migahawa na biashara zinginezo
Ghala za vyakula ,watoa misaada ya chakula ,wasambaza chakula au miradi ya kupambana na njaa
Kampeini zinazohamasisha ustawi kwa mifugo inayotunzwa kwa wingi kwenye eneo dogo
Matumizi ya wanyama au ufugaji wa wanyama
Miradi inayohusisha matumizi ya bidhaa za wanyama (vyakula vitokanayo na wanyama , ngozi n.k )
Vyama vya siasa au uidhinishaji wa mgombea
Masomo ya ziada , utafiti kwa wanafunzi , ada ya chuo kikuu n.k
Taasi yako inafanya kazi zake ndani ya Marekani au tawi la taasisi ya kimataifa iliyoko nchini Marekani
Taasisi kubwa za kimataifa na matawi yake